Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:45

Magenge yenye silaha Nigeria yatangazwa ni makundi ya ugaidi


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (Facebook/ Muhammadu Buhari)
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (Facebook/ Muhammadu Buhari)

Serikali ya Nigeria imetangaza rasmi kwamba makundi yenye silaha yanayotekeleza harakati zao nchini humo ni makundi ya kigaidi.

Magenge hayo yamekuwa yakitambuliwa kama majambazi.

Hatua hiyo inajiri mwezi mmoja baada ya mahakama kuu mjini Abuja kutoa uamuzi kama huo kuhusu magenge hayo.

Magenge hayo ya uhalifu yanayodhibithi sehemu kubwa nchini Nigeria, yamewateka nyara wanafunzi wa shule, kuwapiga na kuwateka nyara watu, kuwabaka na kuwalazimisha baadhi ya waathirika kuwa makahaba au watumwa wa ngono.

Hatua ya kuyatambua magenge hayo kuwa magaidi yanatoa mamlaka kwa jeshi la Nigeria kupambana nayo.

Majimbo ya kaskazini magharibi na sehemu za kati kaskazini, yameathiriwa kwa muda mrefu na magenge hayo yanayotekeleza mashambulizi kila mara.

Magenge yenye silaha nziti nzito yamekuwa yakiiba mifugo, kuwateka watu nyara na kutaka kulipwa pesa ili kuwaachilia huru.

Mashambulizi yameongezeka sana katika siku za karibuni, shinikizo limeongezeka kwa serikali kuu, ambayo tayari inapambana na kundi lenye silaha la bokoharam na makundi mengine upande wa kaskazini mashariki kwa aidi ya muongo mzima, ili kujaribu kusitisha mashambulizi hayo.

XS
SM
MD
LG