Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 03:27

Watu 45 wauawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji Nigeria


Ramani ya Nigeria barani Afrika

Ofisi ya rais wa Nigeria imesema kwamba darzeni ya watu wameuawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Nasarawa, katikati mwa nchi hiyo.

Katika taarifa, Ofisi ya rais Muhammadu Buhari imesema kwamba wakulima 45 wameuawa katika mapigano hayo yaliyoanza ijumaa. Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Buhari ameelezea masikitiko makubwa kutokana na mauaji hayo na kusema kwamba serikali itahakikisha kwamba wahusika wanashitakiwa.

Polisi katika sehemu hiyo wamesema kwamba mapigano yalianza pale wafugaji kutoka jamii ya Fulani waliposhambulia vijiji vinavyokaliwa na watu wa jamii ya Tiv, baada ya kifo cha mtu kutoka kwenye jamii yao, wakidai kwamba kimesababishwa na wakulima.

Msemaji wa polisi wa Nasarawa Ramhan Nansel amesema kwamba wanajeshi wametumwa sehemu hiyo kurejesha hali ya utulivu na kuwakamata wahusika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG