Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:20

Maelfu ya Waethiopia wajitokeza Addis Ababa kulaani vikwazo vya Marekani


Waandamanaji wanaoiunga mkono serikali ya Ethiopia wapinga hatua ya vikwazo ya serikali ya Marekani kwa madai ya uvunjifu wa haki za binadamu yanayofanya huko Tigray, mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 30, 2021.
Waandamanaji wanaoiunga mkono serikali ya Ethiopia wapinga hatua ya vikwazo ya serikali ya Marekani kwa madai ya uvunjifu wa haki za binadamu yanayofanya huko Tigray, mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 30, 2021.

Maelfu kwa maelfu ya Waethiopia walikusanyika kwenye uwanja mkubwa wa michezo mjini Addis Ababa kulaani uingiliaji kati kutoka nje, hasa hatua ya Marekani kuiwekea serikali vikwazo vya kiuchumi.

Pia wamepinga kitendo cha Marekani kuzuia msaada wa kijeshi kutokana na ghasia zinazoendelea katika jimbo la Tigray.

Waandamanaji walikusanyika kutokana na wito wa serikali wakibeba mabango yanayolaani vikwazo hivyo vya Marekani na uingiliaji kati wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi yao.

Mkusanyiko huo mkubwa pamoja na maandamano mengine madogo katika baadhi ya miji ya Ethiopia yalipangwa na Wizara ya Masuala ya Wanawake, Watoto na Vijana chini ya kauli mbiu : sauti zetu kwa ajili ya uhuru wetu na utawala wetu.

Marekani ilitangaza wiki hii inaanza kuzuia kuwapa visa maafisa wa serikali na jeshi wa Ethiopia na Eritrea wanaochukuliwa wanahujumu juhudi za kutanzua mapigano ya Tigray. Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imelaani vikwazo hivyo vya Marekani na kueleza ni kitendo cha kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG