Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:40

Janga la kibinadamu laendelea Tigray


Wakimbizi kutoka Tigray, Ethiopia wasubiri kupata msaada katika kambi moja kwenye mpaka wa Sudan
Wakimbizi kutoka Tigray, Ethiopia wasubiri kupata msaada katika kambi moja kwenye mpaka wa Sudan

Mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa eneo la Tigray nchini Ethiopia  linaloshuhudia ghasia liko katika hali mbaya, ambapo watu wanafariki kutokana na njaa huku ubakaji ukiendelea pamoja na ukosefu wa huduma muhimu za afya.

Hayo amesyasema Jumatatu wakati akihutubia wanahabari na kuongeza kuwa takriban watu milioni tano kutoka eneo hilo wanahitaji misaada ya dharura na hasa chakula.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Novemba mwaka uliyopita alituma vikosi vya serikali kuu kwenye eneo hilo akidai kuwa wapiganaji kutoka chama cha Tigray People's Liberation, TPLF walikuwa wameshambulia kambi za jeshi.

Kiongozi huyo ambaye pia aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel alitangaza ushindi baadaye mwezi huo baada ya wanajeshi wake kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Tigray, Mekele.

Hata hivyo mapigano yanaendelea miezi 6 baadaye huku kukiwa na madai ya mauwaji pamoja na ubakaji kutoka kwa viosi vya serikali pamoja na vile kutoka nchi jirani ya Eritrea.

XS
SM
MD
LG