Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:27

Marekani inasubiri ripoti ya Ethiopia na Tigray


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price

Marekani inasuburia ripoti ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na manyanyaso katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia, Tigray, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price, ameuambia mkutano na wanahabari kwamba Marekani ina wasiwasi mkubwa kuhusu vitendo vya mauaji yaliyofichuliwa wiki iliyopita na vyombo vya habari vya CNN na BBC yaliyotekelezwa na vikosi vya Ethiopia.

Amesema kwamba Marekani inaangalia kwa ukaribu ripoti hizo na inashutumu vikali mauaji watu kufurushwa makwao kwa kulazimishwa manyanyaso ya kingono, na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu ambao mashirika mbalimbali yameripoti kutokea.

Licha ya kueleza hayo yote, Price hakuweka wazi kuhusu nini Marekani inaamini aliyetekeleza ukiukwaji huo wa haki za binadamu.

Bwana Price amepokea ahadi ya Ethiopia kuwa vikosi vya Eritrea vitaondoka Tigray, na kuuita uamuzi huo kuwa juhudi muhimu katika kuondoa mgogoro uliopo katika eneo hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia amesema uchunguzi wa pamoja na Wataalamu kutoka nje kuhusiana na shutuma za kukiukwa haki za binadamu utaanza haraka.

Ethiopia ambalo ni taifa la pili Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu, inakabiliwa na mvutano wa makabila yasiyopatana yakigombania ardhi, madaraka, na rasilimali wakati huu ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Juni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG