Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:52

Maduro aamrisha mpaka Venezuela ufungwe kuzuia Guaido asiingize misaada


Rais Maduro (kulia) na Rais Guaido wanaopingana Venezuela
Rais Maduro (kulia) na Rais Guaido wanaopingana Venezuela

Rais Nicolas Maduro ameamrisha kufungwa kwa mpaka wa Venezuela unaopakana na Brazil Alhamisi.

Wakati huohuo mvutano wa madaraka ukiendelea kati yake na Huan Guaido, kiongozi wa upinzani anayeendeleza juhudi za kuingiza msaada wa kibinadamu nchini humo licha ya kuzuilia na jeshi.

Guaido amekuwa yumo katika msafara wa magari yaliyoingia Colombia kubeba msaada uliotolewa na Marekani, akikaidi amri ya jeshi la Maduro, linalomzuia kuleta misaada hiyo ya kibinadamu Venezuela.

Maduro hata hivyo amekataa msaada wa kibinadamu uliokuwa umetolewa kupitia ombi la Guaido kwa madai ya kwamba ni njama inayotumiwa na utawala wa Marekani kuingia nchini humo kijeshi.

Lakini Guaido ameapa ataendelea na juhudi za kuingiza msaada huo nchini Venezuela na ifikapo Jumamosi misaada hiyo itakuwa imeingizwa nchini.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG