Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 09:46

Madaktari : Wapalestina 200 wajeruhiwa katika mapambano na polisi wa Israeli


Wapalestina wakijihami kutokana na maguruneti ya polisi wa Israeli katika ghasia nje ya msikiti wa Al-Aqsa.

Wapalestina na polisi wa Israeli wamepambana usiku mzima wa Ijumaa kuamkia Jumamosi kwenye uwanja wa msikiti wa Al-Aqsa na sehemu nyingine za Jerusalem.

Mapambano hayo yamesababisha idadi ya Wapalestina waliojeruhiwa kuongezeka na kufikia zaidi ya 200, madaktari wamesema Jumamosi, wakati jiji hilo likijitayarisha kwa ghasia zaidi baada ya wiki kadhaa za kukosekana utulivu.

Maandamano wakati wa usiku yalianza tangu mwezi mtukufu wa Ramadhan kuanza kutokana na masharti yaliyowekwa na polisi katika eneo maarufu wanapokutana watu na limeibua hasira katika siku za karibuni kutokana na vitisho vya kuwahamisha darzeni za Wapalestina kutoka majumbani mwao mashariki mwa Jerusalem, inayodaiwa na pande zote katika mgogoro wenye kuendelea kwa miongo kadhaa.

Haikufahamika kile kilichoanzisha vurugu katika msikiti wa Al-Aqsa, ambapo kulizuka ghasia wakati Polisi wa Israeli wakiwa wamevalia vifaa vya kuzuia ghasia walipelekwa kwa idadi kubwa huku maelfu ya Waislam waliokuwa wanafanya ibada walikuwa katika sala ya jioni katika eneo lenye mnyanuko.

Wapalestina wanajihami kutokana na guruneti zilizofyatuliwa na polisi wa Israeli wakilenga kuwasambaza Wapalestina waliokuwa wamekusanyika katika lango kubwa la Damascus kuingia Mji wa Zamani wa Jerusalem baada ya mapambano kutokea katika viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa Mei 7, 2021.
Wapalestina wanajihami kutokana na guruneti zilizofyatuliwa na polisi wa Israeli wakilenga kuwasambaza Wapalestina waliokuwa wamekusanyika katika lango kubwa la Damascus kuingia Mji wa Zamani wa Jerusalem baada ya mapambano kutokea katika viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa Mei 7, 2021.

Usiku wote makundi makubwa ya waandamanaji walionekana wakitupa mawe huku polisi wa Israeli wakiwafyatulia risasi za mpira na maguruneti.

Muda fulani, polisi waliingia katika moja ya majengo katika uwa la Al-Aqsa, ambapo kuna msikiti wa Al-Aqsa na eneo la Sanaa ya dhahabu ya kihistoria.

Shirika la huduma za dharura la Mwezi Mwekundu la Palestina limesema watu waliojeruhiwa 88 wamelazwa hosptali.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema watu 83 walijeruhiwa kwa risasi za mpira, kati yao watatu waliopigwa katika jicho, wawili wakiwa na majeraha hatarishi kichwani na wawili taya zao zimevunjika.

Polisi wa Israeli wamesema waandamanaji walikuwa wanatupa mawe, baruti za moto na vitu vingine kuwalenga wao, na kuwajeruhi maafisa 17, nusu yao wamelazwa hospitali. “Tutajibu mashambulizi hayo kwa nguvu zote kwa ghasia zote za uvunjifu wa amani, vurugu na mashambulizi dhidi ya jeshi letu,”imesema katika tamko lake Ijumaa jioni.

Uwa la Msikiti wa Al-Aqsa ni sehemu ya tatu takatifu zaidi katika Uislam. Pia ni sehemu takatifu zaidi kwa Wayahudi, wanaoiita kama Temple Mount kwa sababu ilikuwa ni sehemu ya makanisa ya kihistoria ya dini ya Kikristo.

Takriban waumini 70,000 walihudhuria katika sala ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhan katika msikiti wa Al-Aqsa, ofisi ya Kiislam inayosimamia uwa hilo imesema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG