Watu 57 waliuawa wakati treni ya abiria iliyojaa wanafunzi ilipogongana na treni ya mizigo tarehe 28 mwezi Februari, mwaka wa 2023, karibu na bonde la Tempi katikati mwa Ugiriki.
Miaka miwili baadaye, changamoto za kiusalama zilizosababisha ajali hiyo hazijatatuliwa, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika. Uchunguzi tofauti wa mahakama bado haujakamilika, na hakuna mtu aliyepatikana na hatia katika ajali hiyo.
Maandamano makubwa yalipangwa katika miji mingi nchini kote. Safari zote za ndege za kimataifa na za ndani zilisitishwa, huku wadhibiti wa safari za anga wakiungana na mabaharia, madereva wa treni, madaktari, wanasheria na walimu katika mgomo mkubwa wa saa 24 ili kutoa heshima kwa wahanga wa ajali hiyo. Biashara zilifungwa na kumbi za sinema zikafuta maonyesho.
Forum