Wachunguzi kutoka taasisi tofauti za Marekani wamepata kisanduku kinachonasa mawasiliano kati ya rubani na waelekezi wa ndege kinachojulikana kama Black Box, kutoka kwenye ndege ya shirika la American, ambayo ilivunjika katika vipande kadhaa na kuanguka katika mto Potamac, baada ya kugongana na helikopta ya kijeshi ya Marekani.
Bodi ya taifa inayosimamia usalama wa safari itakusanya taarifa kutoka kwenye vifaa vya kunasa mawasiliano vya ndege hiyo ili kubaini kilichopelekea ajali hiyo.
Hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo iliyotokea karibu na uwanja wa ndege wa kitaifa wa Ronald Reagan.
Kuna ripoti kwamba kulikuwa hakuna wafanyakazi wa kutosha kuelekeza ndege wakati wa ajali hiyo na kwamba mtu mmoja alikuwa anafanya kazi ya watu wawili.
Forum