Uchaguzi huo unafanyika baada ya kutokea mashambulizi, ya hivi karibuni yakiwa Munich, na mjadala mkubwa umehusu uhamiaji.
Chama cha AfD kimepata uungwaji mkono kutoka kwa bilionea Elon Musk, mshirika mkubwa wa rais wa Marekani Donald Trump.
Lakini msimamo wa chama hicho umeonekana kutowavutia wajerumani. AfD kinachunguzwa na idara ya ujasusi ya Ujerumani kwa madai ya kuwa na itikadi kali na maandamano dhidi ya wanasiasa wenye msimamo mkali yamekuwa yakiendelea Berlin na miji mingine.
Hali mbaya ya uchumi ilipelekea kuanguka kwa serikali ya muungano wa vyama vitatu, mnamo mwezi Novemba.
Kansela wa sasa Olaf Scholz, wa Social demokrats, anataka kukopa pesa zaidi ili kujaza pengo la bajeti na kuisaidia Ukraine kivita, lakini Fredrich Merz, kiongozi wa Christian Democrats, anasema Ujerumani haistahili kukopa zaidi.
Forum