Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 13:29

Maandamano dhidi ya kodi mpya, kujiuzulu Waziri Mkuu Jordan


Waandamanaji wakikabiliana na polisi wa kuzuia ghasia Amman, Jordan, Juni 2, 2018.

Waziri Mkuu wa Jordan amejiuzulu, baada ya siku nne za maandamano yanayopinga sheria ya kodi mpya ya mapato.

Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Jordan Hany al Mulki Jumatatu kulitokana na maandamano ya siku nne mfululizo katika miji mikuu na miji mingine nchini, na maandamano hayo pia kujikita nje ya ofisi ya waziri mkuu katika mji mkuu Amman.

Vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu vimeripoti kuwa Waziri wa Elimu Omar Razaz ametakiwa na Mfalme Abdallah kuunda serikali mpya.

Al Mulki alikuwa amesisitiza kuendelea kuwasilisha muswada wa kodi mpya ya mapato, pamoja na kuendelea kuwepo maandamano nchini kote.

Amesema kuwasilisha muswada huo kwa ajili ya kujadiliwa bungeni hakumaanishi kwa namna yoyote ile kwamba bunge limeukubali muswada huo wote au sehemu yake.

Serikali ilikuwa inajaribu kusukuma ongezeko la kodi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa mkopo unaotolewa na Shirika la Fedha Duniani.

Jordan hivi sasa inadeni la takriban Dola za Kimarekani bilioni 40. Ongezeko la kodi katika mafuta, umeme na maji, pamoja na mpango wa kodi mpya ya mapato umesababisha hasira kubwa kwa wananchi.

Mkuu wa Polisi wa Jordan Fadel al Hamoud amesema Jumatatu watu kadhaa wamekamatwa wakati wa maandamano hayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG