Marekani bado inaendelea kuwa juu kwenye orodha ya janga hili, ambapo kuna maambukizi takribani milioni 20 na vifo 345,000 vya virusi vya Corona, John Hopkins iliripoti.
India ina kesi milioni 10.2 na zaidi ya vifo 148,000, huku Brazil ikiwa na kesi milioni 7.6 na karibu vifo 195,000 kulingana na ripoti ya John Hopkins.
Watu 42 katika jimbo la West Virginia nchini Marekani walidhani wamepatiwa chanjo ya virusi vya Corona, lakini badala yake walipewa chanjo ambayo kile gazeti la The New York Times ilichofafanua kama matibabu ya majaribio ya kinga-mwili ya Monoclonal.