Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 21:56

Rais mteule wa Marekani apewa chanjo ya Covid-19


Rais mteule wa Marekani Joe Biden apewa chanjo dhidi ya Covid-19 mjini Newark,Delaware ,Jumatatu.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden jana Jumatatu amepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona wakati akitazamwa moja kwa moja kwenye televisheni ili kushawishi wamarekani kuwa zoezi hilo ni salama.

Kabla ya kupokea chanjo hiyo, Biden alionekana akijiandaa na kisha kumweleza muuguzi kuendelea na shuguli wakati akiwa kwenye hospitali moja mjini Newark, Delaware. Mkewe Jill Biden saa kadhaa kabla pia alipokea chanjo kwenye hospitali hiyo ambayo iko karibu na kwao nyumbani. Baadhi ya viongozi wengine mashuhuri wa Marekani waliopokea chanjo hiyo tayari ni pamoja na makamu wa rais Mike Pence, spika wa bunge Nancy Pelosi na kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la senate Mitch McConnell. Rais wa Marekani Donald Trump ambaye mwezi Oktoba alipatikana kuwa na virusi vya corona kufikia sasa hajasema ni lini amepanga kuipokea. Marekani inaongoza ulimwenguni kwenye idadi ya maambukizi huku tayari ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo 318,000 kutokana na Covid-19 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Imetayarishwa na Harrison Kamau.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG