Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 13:32

Watoto robo milioni wako hatarini kuathiriwa na magonjwa hatarishi


Mwanamke akipita katika vibanda vilivyoko katika kambi ya 25 de Junio wanakoishi watu waliolazimika kikumbia maeneo yao huko Metuge Disemba 9, 2020 kutoka eneo la magharibi la Cabo Delgado.

Watoto robo milioni wasiokuwa na makazi nchini Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado ambalo limekumbwa na ghasia wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ambayo yataharisha maisha yao, huku msimu wa mvua ukiwa umeanza, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limeonya. 

Watoto ni karibu nusU ya zaidi ya watu 530,000 ambao wamelazimika kukimbia makazi yao wakati ghasia zinasambaa katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

UNICEF inasema watoto wamekabiliwa na hatari nyingi katika muda wa miaka miwili iliyopita, ikiwemo kimbunga, mafuriko, ukame na hali ngumu ya uchumi ambayo imesababishwa na janga la Covid 19.

Msemaji wa UNICEF, Marixie Mercado ameiambia VOA kuwa watoto hawa hivi sasa wanatishiwa na mlipuko magonjwa mabaya yatokanayo na mji, kama vile kuharisha na kipindupindu na kusambaa zaidi kwa virusi vya corona. Anasema watoto wenye utapiamlo mbaya sana, hasa ndiyo walio katika hatari zaidi.

“Utapiamlo mbaya sana unaweza kuchangia katika hali ya kutishia maisha, hasa kwa watoto ambao tayari ni wagonjwa wana malaria au surua, magonjwa ambayo yapo huko Cabo Delgado. Kwahiyo, watoto ambao wanaathiriwa na matatizo m,engine wana nafasi mara tisa au 10 kufariki kama ilivyo kwa mtoto wa kawaida mwenye utapiamlo mbaya sana,” Mercado amesema.

FILE - Wanawake na watoto waliosambaratishwa katika eneo la Centro Agrrio de Napala, ambapo mamia ya walio lazimika kukimbia makazi yao waliwasili hivi karibuni, wakikimbia vita katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji Disemba 11, 2020.
FILE - Wanawake na watoto waliosambaratishwa katika eneo la Centro Agrrio de Napala, ambapo mamia ya walio lazimika kukimbia makazi yao waliwasili hivi karibuni, wakikimbia vita katika jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji Disemba 11, 2020.

UNICEF inasema watoto wawili kati ya kila watoto watano katika jimbo hilo wana utapiamlo sugu. Mercado anaelezea kuwa watoto hawa wanahitaji tiba maalum na huduma nzuri ili waweze kuishi.

UNICEF, anasema, inapeleka huduma za timu ambazo zinahama kutoka sehemu moja hadi nyingin kwa ajili ya lishe bora na kutoa matibabu kwa kesi ambayo ni mbaya sana.

“Pia, nadhani tuna wasi wasi mkubwa sana kuhusu watoto ambao wamejikuta katika hali ya hatari isiyo ya kawaida na wameshuhudia au kukumbwa na manyanyazo ya kimwili na kisaikolojia. Kwa hili, ni muhimu kwamba tuna nguvu ya kuwa na majibu ya ulinzi kwa watoto hawa, ambayo yanajumuisha msaada wa kisaikolojia na huduma ya muda mrefu.” Amesema Mercado.

UNICEF inaomba karibu dola milioni 53 ili kujibu mahitaji ya haraka ya kibinadamu nchini Msumbiji katika mwaka ujao. Inajukuisha kiasi cha dola milioni 30 kwa ajili ya mahitaji makubwa sana huko Cabo Delgado.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG