Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:43

Ufaransa yaanza kuruhusu watu kutoka Uingereza kuingia nchini


Eneo la ukaguzi la Pit Stop linalounganisha nchi za Ulaya ambapo malori yanakaguliwa kabla ya kuanza safari kutoka Ufaransa kwenda Uingereza, Dec. 22, 2020.
Eneo la ukaguzi la Pit Stop linalounganisha nchi za Ulaya ambapo malori yanakaguliwa kabla ya kuanza safari kutoka Ufaransa kwenda Uingereza, Dec. 22, 2020.

Ufaransa imeanza kuwaruhusu watu kuingia nchini humo kutoka Uingereza siku ya Jumatano.

Hatua hii inafuatia marufuku ya usafiri iliyokuwa imeweka pamoja na nchi nyingine za Ulaya ili kudhibiti aina mpya ya Covid 19 kusambaa.

Wale wanaowasili Ufaransa lazima wawe wamepimwa na kuonekana hawana virusi vya corona na hilo liwe limefanyka chini ya saa 72.

Marufuku siyo tu imesitisha mtitiriko wa watu kote kwenye mipaka, lakini pia imesababisha kuvuruga kwa kiasi kikubwa cha usafirishaji bidhaa kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo imechochea khofu ya kutokea uhaba wa chakula na bidhaa nyingine.

Uingereza, Ufaransa na Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano Jumanne kufungua njia kwa marufuku hiyo kuondolewa.

XS
SM
MD
LG