Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:17

Safari za ndege kuingia na kutoka Uingereza zasitishwa


Uingereza yaweka masharti makali zaidi kutokana na maambukizi ya aina mpya nchini humo. Bango linaloeleza masharti hayo limewekwa na serikali ya nchi hiyo.
Uingereza yaweka masharti makali zaidi kutokana na maambukizi ya aina mpya nchini humo. Bango linaloeleza masharti hayo limewekwa na serikali ya nchi hiyo.

Usafiri wa ndege kuingia na kutoka Uingereza ulisitishwa Jumatatu katika nchi nyingi za Ulaya pamoja na Canadan na Hong Kong.

Hali hiyo imezusha wasi wasi mkubwa katika viwanja vya ndege baada ya baadhi ya nchi hizo kufunga usafiri kwa hofu inayotokana na aina mpya ya virusi vya corona.

Aina hiyo mpya inayotokana na ile inayosababisha ugonjwa wa COVID-19 iligunduliwa kusini mashariki mwa Uingereza na watu kadhaa walioambukizwa na aina hiyo ya virusi wamepimwa huko Denmark, Uholanzi Ubelgiji na Australia.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema hadi hivi sasa hakuna dalili kwamba virusi hivyo vinaambukiza kwa haraka zaidi kuliko vile vya awali lakini utafiti zaidi unabidi kufanyika.

Safari za ndege kutoka nchi za Ulaya kuelekea Uingereza zilisitishwa kwa ghafla Jumatatu na kuzusha hali ya taharuki kwa wasafiri na família zao waliopanga kurudi nyumbani kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anakutana na baraza lake la mawaziri katika kikako cha dharura kujadili suala hilo.

XS
SM
MD
LG