Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 06:54

Maafisa wanne walio jaribu kupindua serikali Gabon wakamatwa


Mwanajeshi aliyejitambulisha kama Luteni Obiang Ondo Kelly akitangaza mapinduzi katika nchi ya Gabon.

Msemaji wa serikali ya Gabon amesema maafisa wa jeshi wote isipokuwa mmoja tu kati ya walioshiriki katika jaribio la kupindua serkali mapema Jumatatu wamekamatwa.

“Wanne wamekamatwa na mmoja amekimbia,” amesema msemaji wa serikali Guy-Bertrand Mapangou.

Maafisa wa jeshi walikiteka kituo cha radio cha taifa kinacho milikiwa na serikali, Jumatatu huko katika mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville,

Wanajeshi hao walieleza dhamiri yao ya kuunda baraza la kitaifa la kuendesha nchi hiyo.

Luteni Kelly Ondo Obiang amesema katka radio hiyo kuwa hotuba ya Rais Ali Bongo alioitoa kupitia radio ya nchi hiyo “ilithibitisha wasiwasi uliopo juu ya uwezo wa rais katika kuendelea kutekeleza majukumu yake.”

Rais huyo yuko Morocco, akiendelea na matibabu baada ya kupata kiharusi.

Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni alipeleka wafanyakazi wa jeshi la Marekani huko Gabon kwa sababu ya kuwepo wasiwasi wa kutokea machafuko katika nchi jirani ya Congo.Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG