Baadhi ya maeneo ya milima ya Rockies na eneo la Midwest tayari yamepata theluji au huenda yakapata theluji mpya Jumatatu, maeneo mengine ya nchi ambayo kwa kawaida yanafunikwa na theluji wakati huu wa mwaka bado yanaonekana kuwa yako nyuma kuwa na mn’garo wa theluji.
“Baadhi ya watu watapata ndoto zao, matakwa yao, na kupata Krismas yenye theluji dakika ya mwisho,” alisema Judah Cohen, mkurugenzi wa utabiri wa hali ya hewa huko katika Kituo cha Utafiti cha Verisk Atmospheric and Environmental Research. “Lakini sehemu nyingi za nchi hii zitakuwa na Krismas ya kawaida isiyokuwa na theluji.”
Kati ya maeneo ambayo yana kawaida ya kupata theluji wakati wa Desemba ni eneo la Northeast, ambako dhoruba kali ilitokea wiki hii na kuleta mvua nyingi katika eneo la michezo ya theluji, ski, ikiondoa theluji iliyokusanyika katika eneo.
“Haikuondoa njia zetu. Lakini ilikuwa ni mvua kubwa,” alisema Tom Day, Manager Mkuu wa Jumba la mapumziko la Gunstock Mountain Resort huko Gilford, New Hampshire.
Alikuwa akicheza katika eneo lenye theluji Jumatatu, wakati likiwa limefungwa, huku mvua yenye kijoto ya sentimeter 8.8 ikinyesha na upepo mkali ukivuma.
“Hilo ni neno lenye herufi nne, rain, katika shughuli zetu,” Day alisema.
Theluji katika maeneo mbalimbali ya Marekani iko chini sana kufuatia rikodi za kipindi hiki kwa mwaka huu, alisema Cohen, ambaye hatarajii kuwepo mabadiliko makubwa wakati wa Krismas.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP
Forum