Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 19:42

Rais Biden awasamehe batamzinga wawili ambao walipelekwa kwa ajili ya mlo wa Thanksgiving


Rais Biden alipowasamehe batamzinga aliopewa kwa jili ya mlo wa Thanksgiving Novemba 20, 2023. Picha na REUTERS/Leah Millis
Rais Biden alipowasamehe batamzinga aliopewa kwa jili ya mlo wa Thanksgiving Novemba 20, 2023. Picha na REUTERS/Leah Millis

Liberty na Bell wanaweza kupanua mbawa zao bila hofu. Siku ya Jumatatu Batamzinga hao wawili walipelekwa White House kwa ajili ya sikukuu ya Thanksgiving sikukuu ya kila mwaka ambayo ni desturi ya White House: rais aliwasamehe batamzinga hao wasiwe chakula cha jioni.

"Ninawasamehe Liberty and Bell. Hongera, ndege," Biden alisema baada ya mmoja wa bata mzinga wa siku ya Thanksgiving kuwekwa kwenye meza karibu naye.

Hafla hiyo, mwaka huu imefanyika katika uwanja wa South Lawn badala ya bustani ndogo ya Rose garden, inaashiria mwanzo usio rasmi wa msimu wa likizo huko Washington, na hususani Jumatatu ilikuwa siku ya ufunguzi wenye shughuli nyingi.

Rais Joe Biden, kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Marekani, pia alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 81 Jumatatu. Mchana, mke wake Jill Biden alipokea mti wa rasmi Krismas kwa ajili ya White House, mti aina ya Fraser wenye urefu wa futi 18.5 (mita 5.6) kutoka Fleetwood, North Carolina.

Biden alifanya utani kuhusu umri wake, akisema, "hii ni kumbukumbu ya miaka 76 ya tukio hili. Nataka ujue kuwa sikuwepo kwa tukio la kwanza." Umri wa mgombea huyo wa chama cha Democrat umezua gumzo wakati akigombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwakani.

Forum

XS
SM
MD
LG