Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:10

Israel na Hamas huenda wakafikia makubaliano


Moshi ukifuka wakati wa shambulio la bomu la Israel huko Rafah Novemba 11, 2023. Picha na SAID KHATIB / AFP.
Moshi ukifuka wakati wa shambulio la bomu la Israel huko Rafah Novemba 11, 2023. Picha na SAID KHATIB / AFP.

Makubaliano kati ya Israel na Hamas kuwaachia darzeni ya mateka wanaoshikiliwa katika maeneo ya wapalestina yanaendelea, kwa mujibu wa ripoti mpya.

Makubaliano kama hayo huenda yakapelekea kuwepo kwa sitisho la muda la mapigano huko Gaza ili misaada inayohitajika sana ivuke mpaka. Maafisa wa Marekani na Israel wanasema hakuna makubaliano yoyote yaliyokamilishwa.

Gazeti la Washington Post limeripoti kwamba Israel na kundi la Hamas ambalo limetajwa na Marekani kuwa ni la kigaidi, wanakaribia kufikia makubaliano ambayo yamesimamiwa na Marekani ya kuachiliwa kwa darzeni ya mateka ambao walichukuliwa na Hamas kwa mabadilishano ya siku tano za sitisho la mapigano ambalo litaruhusu kufikishwa kwa idadi kubwa ya misaada ya kibinadamu.

“Hatujamaliza. Bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa, nadhani huenda ikawa ni mapema mno kusema kwamba makubaliano haya hayaepukiki hasa ukizingatia jinsi tulivyokuwa karibu sana kuliko siku za nyuma.” Alisema Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa, White House Jon Finer.

Na kuongeza “Nadhani jambo moja ambalo hatulishughulikii ni maeneo yote yale ambayo hayajakamilishwa ambapo kuna mashauriano. Hatufanyi mashauriano ya mambo haya hadharani. Lakini ni kipaumbele cha juu sana kuhakikisha yanafanyika. Kuna maendeleo fulani, na tunaweza kutumai kwamba yatafikiwa hatima yake hivi punde ili watu hawa waweze hatimaye kurejea nyumbani.”

Picha ambayo jeshi la Israel linaripoti kuwa ya wapiganaji wa Hamas waliokuwa wamesimama nje ya chumba alichoingia mmoja wa mateka katika hospitali ya Al-Shifa, Novemba 7. Picha na Jeshi la Israel / AFP
Picha ambayo jeshi la Israel linaripoti kuwa ya wapiganaji wa Hamas waliokuwa wamesimama nje ya chumba alichoingia mmoja wa mateka katika hospitali ya Al-Shifa, Novemba 7. Picha na Jeshi la Israel / AFP

Jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi huko Gaza tangu Hamas kuishambulia nchi yao Oktoba 7. Takriban watu 1,200 waliuawa katika shambulizi hilo kwa kile kinachoaminika ni watu 240 walichukuliwa mateka, na wengi bado hawajapatikana.

Naye Balozi wa Israeli nchini Marekani, Michael Herzog alisema “Tuna matumaini kwamba tunaweza kupata idadi kubwa ya mateka watakaoachiliwa katika siku zijazo. Sitaki kuelezea kwa kina kuhusu maelezo ya fursa nzuri kwa makubaliano haya. Lakini kuna juhudi kubwa sana, na nina matumaini kwamba tunaweza kuwa na makubaliano katika siku zijazo."

Katika wiki zijazo kufuatia Oktoba 7, mashambulizi ya anga na ardhini ya Israel yameua zaidi ya wapalestina 12,000 – wengi wao raia – kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Ukingo wa Magharibi.

Shirika la Umoja wa Taifa la Misaada na Ujenzi kwa Wakimbizi wa Palestina au UNRWA linakadiria kiasi cha watu elfu 90 wasiokuwa na makazi wanapatiwa hifadhi katika maeneo yao kote huko Ukanda wa Gaza – idadi ikiwa ni juu zaidi kuliko walivyopanga katika hali ambayo si ya kawaida.

Madaktari wa Kipalestina wakiwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wao, waliohamishwa kutoka hospitali ya Al Shifa Novemba 20, 2023. Picha na SAID KHATIB / AFP
Madaktari wa Kipalestina wakiwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wao, waliohamishwa kutoka hospitali ya Al Shifa Novemba 20, 2023. Picha na SAID KHATIB / AFP

Shirika la Afya Duniani linaripoti kuwa kituo kikubwa sana cha matibabu huko Gaza, Hospitali ya Shifa, kimetapakaa mabaki ya dawa na uchafu na kimekuwa ni kaburi ambalo lina takriban miili 80 nje ya jengo hilo.

Lakini juhudi za karibuni za WHO na Umoja wa Mataifa zimefanikiwa kuwaokoa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao kutimia na kupelekwa kwenye kituo cha matibabu upande wa kusini.T

Thomas White, Mkurugenzi wa UNRWA, huko Gaza alisema “Kwa wengi wao, wanafikiria jinsi ya kuzihudumia familia zao”.

“Lakini ongezeko la watu linatia wasi wasi kuhusu mustakbali wao utakuwaje. Watakwenda kuishi wapi? Watapata wapi sehemu ya kuwapatia watoto wao elimu? Wana mustakbali kwa siku za usoni? Na hilo ni swali kubwa katika mawazo ya watu wa Gaza hivi sasa.” Aliongeza mkurugenzi huyo wa UNRWA.

Mapambano ya kila upande kati ya Israel na Hamas hivi sasa yao katika wiki ya sita na kuna misaada michache tu ya kibinadamu ambayo imewafikia raia wa Palestina ambao wamejikuta katikati ya mapigano.

Kwa wao, sitisho la mapigano huenda likawa na maana ya tofauti kati ya vifo na vifaa vya kuokoa maisha ambavyo vimevuka mpaka.

Forum

XS
SM
MD
LG