Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:35

Dhoruba kubwa ya baridi kupiga Marekani kabla ya sikukuu ya Krismas


Picha ya theluji na baribi kali
Picha ya theluji na baribi kali

Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa ilitoa onyo la dhoruba ya theluji kwa sehemu kubwa sana ya eneo la magharibi kati. Theluji inatarajiwa kunyesha kwa kiwango kikubwa na kuvuka sentimeta 30, inatarajiwa kutoka zaidi katika eneo Great Lakse hadi siku ya Ijumaa.

Mfumo kama huo ulieleza kuwa sentimeta kadhaa za theluji ilinyesha huko Seattle katika eneo la Washington, na kufanya iwe vigumu kuendesha na kusababisha uchelewesho wa safari za ndege na nyingine kufutwa jana Jumanne.

Nje ya Seattle, theluji kubwa ilitarajiwa katika eneo la Cascades mpaka mapema leo Jumatano.

Sentimeta 30 za theluji huenda ikanyesha katika sehemu za milimani huko katika kaunti za King, Snohomish, Pierce na Lewis, kwa mujibu Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa ambayo imeonya “usafiri utakuwa mgumu sana."

XS
SM
MD
LG