Matokeo ya awali yanaonyesha Rais Roche Marc Kabore akiongoza katika uchaguzi wake.
Wagombea urais wa upinzani wamedai kuwepo na wizi wa kura huku Rais Kabore akitarajiwa kushinda kwa muhula wake wa pili katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi, Newton Ahmed Barry amewaambia waandishi wa habari leo kwamba kati ya watu 300,000 hadi 350,000 hawakupiga kura kutokana na hofi za usalama.
Ulinzi ulikuwa mkali kote nchini na karibu asilimia 20 ya nchi nzima haikushiriki kwenye uchaguzi kutokana na vitisho vya wanamgambo. Wengi kati ya wagombea 12 wa upinzani wanamkosoa Rais Kabore kwa kushindwa kukabiliana na mashambulizi hayo.
Mashambulio ya kikatili yanayo fanywa na makundi yanayo tokana na Al-Qaida na kundi la Islamic State yamelazimisha zaidi ya raia milioni moja kuhama makazi yao katika kipindi cha mwaka mmoja peke yake.
Facebook Forum