Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:56

Korea Kaskazini yaendeleza majaribio ya makombora


Watu wakifuatilia kupitia luninga majaribio ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini katika kituo cha treni Seoul Jan. 25, 2022. Photo by Jung Yeon-je / AFP)
Watu wakifuatilia kupitia luninga majaribio ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini katika kituo cha treni Seoul Jan. 25, 2022. Photo by Jung Yeon-je / AFP)

Korea Kusini imesema Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili zaidi ikiufanya mwezi Januari kuwa wenye harakati nyingi zaidi kwa ufyatuaji wa makombora Korea Kaskazini.

Jeshi la Korea Kusini limesema kaskazini ilifyatua kile kinachodhaniwa kuwa makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea baharini upande wa mashariki.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa makombora hayo yamefyatuliwa kutoka eneo karibu na Hamhung mji ulioko ufukweni mwa Korea Kaskazini na yalisafiri kilomita 190 kwa urefu wa kilomita 20.

Hadi sasa Korea Kaskazini imefanya mizunguuko sita ya majaribio na kufyatua takriban makombora kumi katika eneo.

Kwa mujibu wa wachambuzi haya ni makombora mengi yaliyofyatuliwa Korea Kaskazini kwa mwezi mmoja .

XS
SM
MD
LG