Chama cha kinachotawala cha Kiliberali cha Korea Kusini kimemteua mgombea wake kwa uchaguzi wa urais mwaka ujao, kikimchagua mwanasiasa mahiri anayejulikana kwa maoni yake ya wazi ambaye anaweza kuongoza kwenye kinayang’anyiro hicho.
Uteuzi wa Lee Jae-myung Jumapili kama mgombea urais wa Chama cha Kidemokrasia unakuja licha ya juhudi za wapinzani wake kumuonyesha kama mtu hatari na kumuunganisha na kashfa ya nyumba inayoongezeka kwa kasi.
Lee ameapa kupambana na ukosefu wa usawa wa kiuchumi, kuanzisha mapato ya msingi kwa kila mtu na kuanzisha tena miradi ya maridhiano na Korea Kaskazini. Uchaguzi wa Machi mwakani unatarajiwa kuwa mbio mbili kati ya watu wawili Lee na yeyote atakayeshinda uteuzi wa chama kikuu cha kihafidhina mnamo mwezi Novemba.