Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:50

Kipchoge ashinda mbio za marathon Berlin


Mshindi wa Olympic wa Kenya Eliud Kipchoge ameendelea kuithibitishia dunia kwamba yeye ndiye hivi sasa mkimbiaji bora wa mbio ndefu kwa kushinda mbio za Marathon Berlin Jumapili, lakini hakuweka rikodi ya dunia.

Kipchoge alimaliza mbio hizo nchini Ujerumani katika muda wa saa mbili, dakika tatu na sekunde 32 baada ya kuendeleza juhudi za kumshinda mpinzani wake kutoka Ethiopia Guye Adola, ambaye alimaliza mbio hizo mapema kwa sekunde 14 katika mbio hizo (42.195km, 26.219, min).

Mosinet Geremew alimaliza akiwa mshindi wa tatu, katika muda wa 2:06:12.

“Mazingira ya mbio hizo ilikuwa ngumu, kwa sababu ya mvua, lakini kwa bahati nzuri hakukuwa na upepo mkali,” alisema Kipchoge.

XS
SM
MD
LG