Lapid, kiongozi wa upinzani wa Israel alitoa ushahidi katika kesi moja kati ya tatu zinazomkabili Netanyahu ambaye alikanusha makosa hayo yaliyoletwa dhidi yake.
Katika kesi pekee, inayojulikana kama case 1000 Netanyahu ameshitakiwa kwa ubadhirifu wa mali na kuvunja uaminifu na kwamba yeye na mkewe Sara walipokea zawadi zenye thamani ya karibu dola 195,000 kinyume cha sheria,
Zawadi hiyo ilitoka kwa Arnon Milchan, mzalishaji wa filamu wa Hollywood na raia wa Israel na bilionea wa mfanyabiashara wa Australia James Packer.
Waendesha mashtaka wamesema zawadi hizo ni pamoja na mvinyo na sigara na kwamba Netanyahu alimsaidia Milchan katika ushawishi wa biashara zake. Packer na Milchan hawana mashataka yoyote.
Forum