Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 20:22

Israeli yadai kumuua kamanda wa kundi la Kiislam la Jihad


Mfumo wa ulinzi wa anga ukilihami eneo la Israeli dhidi ya roketi zilizlokuwa zinapigwa kutoka Gaza, eneo la Sderot, Israeli, Mei 10, 2023. REUTERS/Ammar

Milipuko imetanda usiku wa kuamkia leo huko  Ukanda wa Gaza na Israel wakati wanamgambo wa Palestina wakirusha zaidi ya roketi 400 upande wa Israel.

Lakini makombora mengi yalikosa mwelekeo baada ya kuingiliwa na ulinzi wa makombora ya Israel. Israel imesema roketi zake zilikuwa ni za kuangamiza zaidi.

Jeshi la Israel limedai limepiga zaidi ya maeneo 130 usiku kucha, ikiwemo maeneo ya kurushia roketi yanayo simamiwa na makundi ya wanamgambo wa gaza.

Roketi zikirushwa kutoka Gaza kuelekea Israeli Mei 10, 2023. REUTERS/Mohammed Salem
Roketi zikirushwa kutoka Gaza kuelekea Israeli Mei 10, 2023. REUTERS/Mohammed Salem

Pia limedai kumuuwa kamanda wa kundi la Kiislamu la Jihad anayeitwa Ali Ghali.

Wafanyakazi wa afya katika mji wa Gaza waliwakimbiza hosoitali watu waliojeruhiwa na shambulizi hilo la mabomu usiku.

Takriban dazani mbili ya wapalestina ikiwemo wanawake watano na watoto watano wameuwawa tangu mapigano yalipoanza kwa mujibu wa maafisa wa palestina.

XS
SM
MD
LG