Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:02

Israeli yaanzisha upya mashambulizi eneo la Gaza


Moshi na moto ukifuka kufuatia shambulizi la angani lililofanywa na jeshi la Israeli huko Mji wa Gaza Mei 10, 2023.
Moshi na moto ukifuka kufuatia shambulizi la angani lililofanywa na jeshi la Israeli huko Mji wa Gaza Mei 10, 2023.

Jeshi la Israel limesema lilianza tena mashambulizi  huko Gaza Jumatano na kumuua mtu mmoja kulingana na Wizara ya Afya ya eneo la Palestina.

Katika taarifa yake jeshi limesema kwa sasa inaishambulia taasisi ya kigaidi ya Islamic Jihad ambayo inarusha roketi kwenye miundombinu huko ukanda wa Gaza.

Afisa wa Wizara ya Afya ya Gaza ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mtu mmoja amekufa katika mashambulizi hayo.

Mashambulizi ya karibuni kabisa yanakuja siku moja baada ya mashambulizi ya Israeli huko Gaza na kuuwa wanamgambo wa juu wa kundi la jihad na wengine 12, ikiwemo watoto wanne, kwa mujibu wa idadi ya Wizara ya Afya.

Jeshi la Irsael limesema Jumatano mashambulizi ni pamoja na kuwafyatulia risasi wanamgambo waliokuwa wakisafiri kwenda kwenye eneo ambako roketi zinarushwa katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Gaza.

XS
SM
MD
LG