Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:33

Mahakama ya Rufaa Kenya yatupilia mbali kesi ya NASA


Raila Odinga na mgombea mwenza wakipokelewa na IEBC
Raila Odinga na mgombea mwenza wakipokelewa na IEBC

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imebatilisha uamuzi wa mahakama uliokuwa umezuia kampuni ya Al Ghurair ya Dubai kuchapisha karatasi za kupiga kura za urais.

Mahakama hiyo ya pili ya ngazi ya juu nchini Kenya Jumanne imesema kuwa Mahakama ya chini ilifanya makosa kwa kutoa amri kusitisha uchapishaji huo kwa sababu ya kuwashirikisha wananchi.

Majaji walitoa uamuzi kuwa kushirikishwa wananchi katika mchakato huo wa kutoa tenda sio sharti katika manunuzi ya moja kwa moja, utaratibu ambao ulitumiwa na tume ya uchaguzi katika kuipa mkataba huo Al Ghurair.

Pia waliikosoa Mahakama hiyo kwa kushindwa kutambua kuwa muda ulikuwa finyu mno kuweza kushughulikia kutoa tenda nyingine.

Hata hivyo, majaji wa mahakama ya rufaa walikubaliana na wale wenzao wa Mahakama ya chini kutupilia mbali madai kuwa Rais Kenyatta alikutana na maafisa wa Al Ghurair na alitumia nafasi yake ya urais kuwapa tenda hiyo.

Mahakama hiyo, wamesema, ilikuwa sahihi kuweka msimamo kuwa vipande vya magazeti haviwezi kutosheleza kuthibitisha kwamba Rais alikutana na wakurugenzi wa kampuni hiyo.

“Makala hizo zinabakia kuwa uvumi mpaka pale mwandishi atapoweza kutokea mahakamani na kuhojiwa juu ya ukweli wa habari hizo,” wamesema.

XS
SM
MD
LG