Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 14:12

Wakenya watatu wahukumiwa kifo kwa kumvua mwanamke nguo


Wanawake wa Kenya waandamana kupinga udhalilishwaji unaotekelezwa na baadhi ya makundi ya watu yanayopinga jinsi walivyovalia nguo zao.

Mahakama moja ya Nairobi, siku ya Jumatano iliwahukumu wanaume watatu kunyongwa, baada ya kupatikana na hatia ya kumvua nguo mwanamke mmoja, kumdhalilisha na kujaribu kumbaka.

Kisa hicho kiltokea wakati wa wimbi la uvamizi wa wanawake miaka mitatu iliyopita, ambapo makundi ya watu yalikuwa yakidai kwamba wanawake walikuwa wanavaa mavazi yasiyokubalika.

Watu hao watatu walikutwa na hatia ya wizi wa kutumia nguvu, ambapo hukumu yake ni kifo.

Hata hivyo, sheria ya adhabu ya kifo nchini Kenya haijatekelezwa tangu mwaka 1987, na hukumu kama hizo zimebadilishwa na kuwa vifungo vya maisha.

Baadhi ya visa vya uvamizi huo, ambavyo vilikithiri mwaka 2014 vilirekodiwa kwanye simu za mkono, na kupelekea maandamano, huku waliokuwa wakipinga vitendo hivyo - wengi wao wakiwa wanawake - wakianzisha hashtag iliyoitwa #MyDressMyChoice kwenye mitrandao ya kijamii.

Muathirika huyo aliiambia mahakama kwamba wanaume hao watatu walikuwa kati ya kundi la wanaume saba waliotaka kumbaka ndani ya basi, lakini wakakaachana naye alipowaambia kwamba alikuwa na virusi vya ukimwi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG