Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 07:48

Mgomo Uganda wakwamisha kesi ya Kaweesi


Washutumiwa wa kesi ya Kaweesi wakifikishwa mahakamani
Washutumiwa wa kesi ya Kaweesi wakifikishwa mahakamani

Kesi ya washukiwa 13 wanaoshutumiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa msemaji wa polisi Andrew Felix Kaweesi imekwama katika mahakama ya Nakawa nchini Uganda.

Hilo limetokea siku ya Alhamisi kufuatia mgomo wa wanaendesha mashtaka wa serikali unaoendelea hivi sasa nchini Uganda.

Kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa katika mahakama ya Nakawa ikisubiri majibu kutoka kwa waendesha mashtaka kuhusu uchunguzi ulipofikia, lakini kutokana na kutokuwepo mahakamani mwendesha mashtaka Apio Caroline ilibidi kesi iahirishwe.

Jumatano waendesha mashtaka wote chini ya kurugenzi ya mashtaka ya umma, nchi nzima, imeingia katika mgomo usiojulikana mwisho wake juu ya mishahara midogo na maslahi duni.

“Kutokana na kutokuwepo mwendesha mashtaka, mahakama haina taarifa kesi imefikia wapi. Sijui kama upelelezi umekamilika ambapo tu nitaweza kupeleka kesi yenu katika mahakama kuu kuzikilizwa. Na kwa sababu hii, sina jinsi yoyote ispokuwa kuwarudisha rumande,” Hakimu wa daraja la kwanza, Noah Saijabi amewaambia watuhumiwa hao na kuahirisha kesi hadi Julai 26.

Watuhumiwa 13 wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Kaweesi na wasaidizi wake wawili; mlinzi Kenneth Erau na dereva Godfrey Wambewo.

Watuhumiwa hao ni Abdul Rashid Mbaziira Buyondo, Mr. Ramadhan Noor Diin Higenyi, Yusuf Mugerwa, Bruhan Baryejusa, Umar Maganda na Ahmed Shafic Ssenfuka.

Wengine ni : Hassan Tumusiime, Ibrahim Kiisa, Othman Muhammad Omerette, Hamid Magando, Abdul Magid Ojegere, Sheikh Musa Abu na Baker Ntanda.

XS
SM
MD
LG