Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 07:31

Kauli ya Rais Mkapa yazua utata Tanzania


Rais mstaafu Mkapa

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema imesikitishwa na matamshi ya Rais Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema imesikitishwa na kauli ya rais wa awamu ya tatu akirudia maneno ya kejeli ya watanzania wenye maoni tofauti na yale ya uongozi wa nchi ulioko madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mkapa alisema hivi karibuni kuwa watu kama hao ni “wapumbavu” na “malofa”.

Kauli hiyo alitamka siku ya Julai 10, 2017 akiwa Chato, Mkoani Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa matamshi ya Mkapa hayapendezi kusikika yakitoka kwa kiongozi wa kitaifa, na ni matamshi yasiyoheshimu maoni tofauti.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG