Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:13

Kesi mbili za kuzuia sera ya utata ya Uingereza zaanza kusikilizwa London


Waandamanaji wakiwa nje ya Mahakama Kuu London, Ijumaa, Juni 10, 2022. (AP Photo/Frank Augstein)
Waandamanaji wakiwa nje ya Mahakama Kuu London, Ijumaa, Juni 10, 2022. (AP Photo/Frank Augstein)

Mahakama za London zimeanza kusikiliza kesi mbili za  dakika za mwisho zilizowasilishwa ili kuzuia  sera yenye utata ya Uingereza ya kuwapeleka wanaoomba hifadhi nchini Rwanda.

Serikali imeahidi kuendelea na mpango wake na kuwahamisha wahamiaji kwa ndege ya kukodisha kesho kupitia uwanja wa ndege ambao haujatangazwa.

Sambamba na Mahakama ya Rufaa, Mahakama ya Juu inasikiliza hoja tofauti kutoka kundi la hisani la Asylum Aid ambalo limefungua kesi ya pili kuizuia serikali kuwasafirisha wakimbizi kwenda Rwanda.

Shirika hilo la msaada limesema mpango wa serikali kutoa siku saba kwa waombaji wa ukimbizi kupata ushauri wa kisheria na kuwasilisha kesi yao ili kuzuiya kurejeshwa ni kasoro na siyo haki.

Kesi hii inasikilizwa na Jaji yule yule ambaye Ijumaa alitupilia mbali kesi ya awali.

Mwezi April serikali ya kikonsevativu ya Waziri Mkuu Boris Johnson ilitangaza kuwapeleka nchini Rwanda wahamiaji ambao hawana vibali, ambako kesi zao za kuomba ukaazi zitasikilizwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kama watafanikiwa wahamiaji hao watabaki Rwanda. Uingereza iliipa Rwanda malipo ya awali ya dola milioni 158 na itatoa pesa nyingine kufuatana na idadi ya watu watakaopelekwa huko.

XS
SM
MD
LG