Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:01

Johnson akabiliwa na tishio la kuondolewa madarakani


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Waziri Mkuu wa Uingereza Jumatatu atakabiliwa na kura ya imani baada ya wabunge wengi katika serikali kwenye chama cha kikosensevativu kuhoji kiongozi huyo wa Uingereza kutumia madaraka vibaya wakati wa kashfa ya “ partygate” .

Tangu mwaka 2019 Waziri Mkuu Johnson alipoteuliwa kushika wadhifa huo amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa na kushindwa kusonga mbele kutokana na ripoti iliyozungumzia sherehe zilizohusisha unywaji pombe wakati Uingereza ikiwa katika masharti ya kufungwa shughuli zake ili kukabiliana na ugonjwa wa COVID -19.

Katika shambulizi kali dhidi ya Johnson ambaye hapo awali hakuweza kupingwa, Jesse Norman kiongozi mwamininifu aliyehudumu kama waziri mdogo katika wizara ya fedha kati ya mwaka 2019 na 2021 alisema waziri mkuu kubakia madarakani ni kuwakashifu wapiga kura na chama.

Ni mmoja wa wabunge wakonsevativu kadhaa aliyepaza sauti yake na kueleza kama Johnson mwenye umri wa miaka 57 amepoteza mamlaka ya kuiongoza Uingereza ambayo inakabiliwa na kudorora kwa uchumi, kuongezeka bei bidhaa na kadhia ya usafiri kufuatia maandamano katika mji mkuu London.

Msemaji wa ofisi ya Johnson, huko Downing Street alisema kura hiyo ni nafasi ya kumaliza miezi kadhaa ya uzushi na itaruhusu serikali kuchora mstari na kusonga mbele ikitoa vipaumbele vya watu.

Graham Brady mbunge mkonsevativu na mwenyekiti wa kamati anaeleza: ” Nimefuata kanuni tulizoziweka. Nilimjulisha waziri mkuu jana kwamba kizuizi kimeondolewa na tukakubaliana na ratiba ya kura ya Imani ifanyike. Alikubaliana na mtazamo wangu, ambao unaendana na kanuni tulizonazo , kwamba kura hiyo zifanyike mapema iwezekanvyo, na hviyo itakuwa leo.”

XS
SM
MD
LG