Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:09

Kerry ana imani ya uchaguzi huru Kenya


John Kerry akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari Kenya Agosti 1, 2017
John Kerry akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari Kenya Agosti 1, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani John Kerry amesema kuwa ana imani ya kuwepo uchaguzi huru Kenya.

“Tuko hapa Ili kuweza kuwasaidia Wakenya, na nina imani kuwa utakuwepo uchaguzi ambao ni wazi, wa haki, huru, na utakao mfanya kila mtu awajibike,” amesema.

Kerry anaongoza Kundi la Wasimamizi wa Uchaguzi la Marekani na pia ni kiongozi mwenza wa Kituo cha Carter, ambacho ni taasisi isiyokuwa ya kibiashara ilioundwa na Rais mstaafu wa Marekani Jimmy Carter.

Amesema ni heshima kubwa kwake kuwa ni sehemu ya kikundi cha waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi wa Kenya.

Kerry pia ameupongeza mhimili wa mahakama wa serikali ya Kenya kwa kazi kubwa ilioifanya katika kutafuta suluhu ya migogoro na kutoa mchakato wa kisiasa ambao utawafanya wajiamini kwenda kupiga kura Jumanne.

“Mwisho wa yote ni juu ya Wakenya kufanya maamuzi na kwa hiyo hilo ni jukumu la watu wa Kenya na viongozi wao kuhakikisha kuna uchaguzi wa amani.

Sote sisi tutatekeleza wajibu wetu na kuwafanya wananchi wajiamini kwenda kupiga kura.

Kerry amempongeza Jaji Mkuu wa Kenya ambaye ameongoza mchakato wa kisheria, ambao ni makini na ulioleta maamuzi na tunafikiria kwa kiwango kikubwa umechangia kuwapa imani watu kuwa tayari kwenda kupiga kura.

XS
SM
MD
LG