Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 26, 2025 Local time: 17:47

Asilimia 25 ya vituo vya uchaguzi Kenya kutotoa matokeo kielektroniki


Mradi wa uhuru wa internet
Mradi wa uhuru wa internet

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC imedokeza kuwa asilimia 25 ya vituo vya kupiga kura havitaweza kupeperusha matokeo kwa njia ya kielectroniki kutokana na matatizo ya mitandao.

Kulingana na afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba vituo elfu 11 havitaweza kutuma matokeo yao kielectroniki kutokana na ukosefu wa mawasiliano ya mitandao kwenye mifumo ya 3G na 4G.

Kutokana na hilo maafisa wa tume hiyo watalazimika kutafuta kule mtandao unapopatikana kabla ya kutuma matokeo kwa njia ya simu za satelait.

Tume hiyo iliamua kutumia mfumo wa kutuma matokeo katika kituo kikuu cha kujumuisha kura kwa njia ya kielectroniki kukabiliana na wizi wa kura.

Kuna jumla ya vituo 40,883 vya kupiga kura nchini ambavyo matokeo yao yatatumwa moja kwa moja hadi kituo kikuu cha kujumuisha kura hizo katika ngazi ya maeneo ya bunge, kaunti na kisha baadae Bomas jijini Nairobi.

Aidha Ezara amesisistiza kuwa jukumu lao katika ngazi ya kitaifa ni kutangaza matokeo ya urais huku maafisa wa tume hiyo katika ngazi ya maeneo bunge na wale katika ngazi ya kaunti wakiachiwa jukumu la kutangaza matokeo ya nyadhifa za Seneta, Mbunge, Gavana, Mwakilishi wa kike katika bunge la kitaifa na mwakilishi wa wadi.

Hii ni baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani iliyopinga hatua ya matokeo hayo kutangazwa katika ngazi ya kitaifa.

XS
SM
MD
LG