Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 21:27

Kenyatta afanya ziara ya kihistoria Somalia


Kenyatta atembelea majeshi ya Kenya nchini Somalia
Kenyatta atembelea majeshi ya Kenya nchini Somalia

Rais Uhuru Kenyatta Jumamosi amefanya ziara ya kihistoria Somalia, na kukutana na vikosi vya Kenya vinavyoshiriki katika jeshi la Afrika la kulinda amani nchini Somalia huko katika kambi ya kijeshi ya Dhobley.

Amiri Jeshi Mkuu wa Kenya akiwa amevalia magwanda ya kivita, alikutana na majeshi ya Kenya na kuwashukuru kwa kujitoa mhanga na kulitumikia taifa lao.

Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Kenyatta kutembelea Somalia katika hali ya kuongeza morali kwa majeshi ya Kenya.

Rais tayari ameshatembelea makao makuu ya Somalia, Mogadishu siku za nyuma katika shughuli za kiserikali.

Rais amewaambia wanajeshi kuwa taifa la Kenya litakuwa siku zote ina deni kwa wanajeshi hao ambao wamekuwa mstari wa mbele kutokomeza vitisho vya al-Shabaab.

“Kuwepo kwenu Somalia kumesaidia watu wengi, na kwa hilo Wakenya wataendelea kuwa na deni la kulipa fadhila kwenu wapiganaji wetu. Kuwepo kwenu Somalia kwa kiwango kikubwa kumewaondoshea watu wetu hofu ya al-Shabaab,” Rais Kenyatta amesema.

Rais amesema; “ Tumeweza kuifufua sekta ya utalii kwa sababu ya ujasiri wenu wa kuifanya nchi yetu iwe na amani.”

Kambi ya Kijeshi ya Dhobley ni makao makuu ya AMISOM, Kituo cha mawasiliano na kumbukumbu muhimu za Umoja wa Mataifa (UN).

XS
SM
MD
LG