Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:54

Kenyatta aongoza katika uchaguzi Kenya


Uhuru na Ruto waonesha stakbadhi za kugombania kiti cha rais
Uhuru na Ruto waonesha stakbadhi za kugombania kiti cha rais

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesema kuwa bado inasubiri kupokea fomu zilizosainiwa rasmi kutoka vituo vyote vya kupigia kura nchini ili kulinganisha na matokeo ya kielektroniki yaliyokuwa yamepeperushwa hapo awali.

Upinzani unaendelea kupinga matokeo yaliyotolewa mpaka hivi sasa, ukisema Alhamisi kuwa ni mgombea wao, Raila Odinga kuwa ndiye mshindi halali.

Mwandishi wa VOA Kenya amesema kuwa Wakenya wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyofanyika Jumanne ambapo Rais aliyoko madarakani Uhuru Kenyatta amegombea dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Mpaka Alhamisi mchana, maafisa wa uchaguzi walikuwa bado wanasubiri kupokea fomu 170 kutoka katika majimbo 290 ya uchaguzi nchini na kiasi cha fomu 1,000 kutoka katika vituo vya kupigia kura 40,883.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka wa Kenya, Wafula Chebukati amesema Alhamisi “hivi sasa tuko katika hatua za mwisho kutoa matokeo.”

XS
SM
MD
LG