Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 14:04

Madaktari 12 wafukuzwa kazi Kenya


Rais Uhuru Kenyatta akihutubia sherehe za Jamhuri Day 2016

Hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi imetangaza kuwaachisha kazi madaktari 12 na kuwapa wengine 48 adhabu kali kwa kususia kufika kazini.

Lakini madaktari sasa wanaeleza kutokata tamaa katika jitihada zao za kuwapa Wakenya picha kamili ya mgogoro huo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Mahakama wiki hii iliwataka magavana na serikali kuafikiana na kutia sahihi stakabadhi tatu ambazo ni muhimu katika mazungumzo hayo.

Lakini baadae katika kongamano la nne la kutupia macho ufanisi na changamoto za mfumo wa ugatuzi mjini Naivasha, Bwana Kenyatta na Gavana Peter Munya kwa niaba ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti walionekana kuwashtumu madaktari kwa kushikilia misimamo mikali na kuzorotesha sekta ya afya.

Masaa machache baada ya matamshi yake, Afisa mtendaji wa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta Lily Koros alitangaza kuwa madaktari kumi na wawili watafutwa kazi na wengine arobaini na nane kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kususia kazi.

Hata hivyo, Daktari Mwachonda Chibanzi ambaye pia ni kiongozi wa muungano huo, amethibitisha kuwa madaktari wenzao wameanza kupokea barua za kufutwa kazi.

lakini amesema kuwa mgomo bado unaendelea mpaka pale serikali itapofahamu vitisho havifai katika mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Mwandishi wetu ameripoti Wakenya wengi walikuwa na matarajio kuwa mgogoro huu ambao umeathiri sana huduma za afya katika hospitali za umma nchini ungepata uvumbuzi wa haraka.

Lakini ameendelea kusema kuwa sasa mgomo huo umefikia hali ambayo hairidhishi.

Pia Katibu Mkuu wa muungano wa madaktari nchini Ouma Oluga alisisitiza kuwa wao wako tayari kufanya mazungumzo ili kupata suluhu.

Mwenyekiti huyo amelaumu kuwa kila wakati muafaka unapoonekana kukaribia kufikiwa, serikali ndio imekuwa ikiendelea kuweka vizingiti.

Katika ripoti ya wapatanishi wa kidini katika mazungumzo haya, serikali ilikuwa imekubali kuongeza marupurupu kwa madaktari kama njia ya kuwafanya madaktari kufutilia mbali mgomo, japokuwa baadaye "ofa" hiyo iliondolewa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG