Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:19

Kenya: Shinikizo laongezeka kwa Rais Ruto kutangaza dharura ya kitaifa nchini


Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto

Shinikizo linaongezeka kwa Rais wa Kenya William Ruto kutangaza dharura ya kitaifa juu ya rekodi mbaya ya ukame katika nchi hiyo hasa upande wa kaskazini mwa nchi ambapo takriban watu milioni tano wameathiriwa.

Mvua kutonyesha kwa msimu wa sita mfululizo kunafanya hali ya njaa kuwa mbaya sana kote katika eneo hilo. Kaunti ya Wajiri, ndiyo imekumbwa vibaya na ukame ambako zaidi ya nusu ya watu huko wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Waathirika wa ukame katika maeneo yaliyokumbwa na ukame wanasubiri kwa hamu misaada katika kijiji cha Kilkiley kwenye Kaunti ya Wajiri. Maelfu ya wafugaji wameweka kambi barabarani ili kutafuta misaada kutoka katika magari yanayopita njiani na makundi ya misaada, akiwemo Rukia Ahmed. Anatengeneza chai kwa ajili ya watoto wake anasema “hatuna chochote cha kupika hivi sasa. Tuko hapa ili kupata msaada, NGOs au watu wanaopita.”

Mamlaka nchini Kenya zinasema mvua kutonyesha kwa msimu wa sita mfululizo kumesababisha mamilioni ya mifugo kufa na kuwaacha Wakenya takriban milioni tano wakihitaji misaada ya kibinadamu.

Zaidi ya nusu ya wale walioathiriwa wako katika kaunti tatu za kaskazini mashariki mwa Kenya – Garissa, Wajir na Mandera.

Kaunti za Wajir, Marsabit na Mandera nchini Kenya
Kaunti za Wajir, Marsabit na Mandera nchini Kenya

Viongozi kutoka eneo hilo wamekuwa wakimuomba rais kutangaza ukame ni janga la kitaifa, lakini wanasema ombi lao halijasikilizwa.

Abass Sheikh, seneta wa Kaunti ya Wajir alizungumza na Sauti ya Amerika alikuwa na haya ya kusema. “Kila mara tunapokutana, tunasema, ‘tangaza’ na rais amekuwa akiahidi, wakati mpaka hivi sasa, bado tunasubiri rais kutangaza ukame ni janga.”

Kama serikali itatangaza ukame ni janga la kitaifa, viongozi wa kieneo wanasema watu wanaweza kupata siku ya kimataifa ambayo wanaihitaji sana.

Mohammed Adow ni mbunge wa Wajir Kusini anasema, “kwsababu ni janga. Watu wanashindwa kupata chakula, mifugo inakufa kwa dazeni kila siku. Nadhani wakati umefika kwa serikalikutangaza ni janga la kitaifa ili tuweze kupata misaada kutoka nje.”

VOA ilimpigia simu mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya rais ili kupata maoni yake lakini hakujibu simu.

Rais wa Kenya William Ruto wiki iliyopita alikiri kuwa hali ya ukame ni mbaya sana na kuahidi misaada zaidi kwenye maeneo yaliyoathiriwa. “Hali ya ukame ni mbaya sna inahitaji majibu ya haraka, hasa uingiliaji kati ili kuepusha kusambaa kwa dhiki na mateso,” ameongezea rais.

Ruto alisema kuwa serikali ya kitaifa imetumia zaidi ya dola milioni 250 kwa program za ukame tangu Septemba mwaka 2021 na imetenga fedha za ziada kutoka katika bajeti ya ziada.

“Katika bajeti ya ziada ya karibuni, tumeweka kando dola milioni 47.2 za ziada kwa ajili ya kujibu hali ya ukame kwa kipindi kati ya Februari na May 2023,” amesema Rais Ruto.

Kwenye kambi, baadhi ya misaada imewasili. Chama cha Msalaba Mwekundu Kenya kimegawa chakula, lakini kwenye kaya chache.

Abdiya Manya ni mratibu wa Msalaba Mwekundi katika ofisi ya Kaunti ya Wajir. “Kama jamii hizi hazitapatiwa msaada wa haraka, hali ni mbaya sana. Chakula kinahitajika sana katika mzozo huu. Jana tulitembelea kambi chache kuzunguka hapa. Baadhi ya watu kutoka maeneo mengine wanafika kutafuta chakula cha msaada hapa. Watu wanalikimbilia gari lolote wanaloliona.”

Wakati huo huo waathirika kama Rukia Ahmed wana chakula kichache sana kama ana chochote, isipokuwa kuna matumaini kwamba msaada wa chakula utafika haraka.

XS
SM
MD
LG