Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:41

Kelly mke wa John Travolta, afariki akiwa na miaka 57


Marehemu Kelly Preston na mumewe John Travolta .
Marehemu Kelly Preston na mumewe John Travolta .

Mcheza filamu maarufu Kelly Preston amefariki akiwa na umri wa miaka 57.

Mume wa Kelly kwa miaka 28, John Travolta, amethibitisha kifo hicho Jumapili jioni baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa miaka miwili, Shirika la habari la Ufaransa AP limeripoti.

Preston alikuwa mpenzi wa fani ya filamu na televisheni kwa miaka mingi na kucheza filamu ikiwemo “Jerry Maguire,” “Twins” na wakati mwengine akishiriki katika filamu alizocheza mumewe kama vile “Battlefield Earth” na “Gotti.”

Wawili hao walioana mwaka 1991 mjini Paris baada ya kukutana katika kucheza filamu na walipata watoto watatu.

Walipata msiba mwaka 2009 baada ya mtoto wao Jett kufa huko Bahamas.

“Upendo wa Kelly na maisha yake yatakumbukwa siku zote,” alisema Travolta katika ujumbe wake wa Instagram.

“Nitatumia baadhi ya muda wangu kuwa na watoto wangu ambao wamempoteza mama yao, hivyo nisameheni mapema iwapo hamtasikia chochote kutoka kwetu kwa muda. Lakini tafadhali tambueni kuwa nitahisi upendo wenu utakao miminika katika wiki na miezi inayokuja wakati tukifarijika na msiba huu.”

Kifo cha Preston kiliripotiwa hapo awali na Jarida la People.

XS
SM
MD
LG