Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 09:39

'Katiba inasuluhisho la mgogoro wa uchaguzi Kenya'


Balozi Robert Godec

Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec kwamba katiba ya Kenya imeweka wazi jinsi gani migogoro inavyowenza kushughulikiwa.

Uvunjifu wa amani lazima usiwepo kabisa katika jumla ya njia za kutafuta suluhisho la migogoro, balozi huyo amewaambia waandishi wa habari nje ya kituo cha kujumuisha matokeo cha Tume ya uchaguzi (IEBC) Nairobi

Lazima kuhakikisha kwamba hakuna Mkenya anapoteza uhai wake kwa sababu ya uchaguzi. Mustakbali wa Kenya ni muhimu zaidi kuliko uchaguzi. Viongozi ni lazima waliweke hilo wazi.

Kila mgombea anatarajia siku moja kula kiapo cha utiifu kwa katiba ya nchi kama mshindi wa chaguzi hizo.

Huu ni wakati viongozi nchi nzima kwenye siasa kuonyesha utiifu wao kwa katiba ya nchi.

Maendeleo ya kidemokrasia ya Kenya yamepatikana kwa tabu kubwa na ni lazima yalindwe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG