Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 15, 2025 Local time: 13:52

IEBC yasubiri fomu mbili kutoa matokeo ya uchaguzi


Wafula Chebukati
Wafula Chebukati

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesema Ijumaa kuwa tayari wamepokea fomu 288 za majimbo 290 ya uchaguzi kwa ajili ya majumuisho ya kura.

Wamesema kuwa hawawezi kutangaza matokeo mpaka wapokee fomu mbili za mwisho zilizokuwa bado hazijawasilishwa. IEBC wanatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wakati wowote Ijumaa.

Wapiga kura Kenya wanasubiri mshindi kutangazwa Ijumaa kufuatia uchaguzi wa urais Jumanne uliompambanisha Uhuru Kenyatta dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Siku ya Alhamisi maafisa wa uchaguzi walikuwa wanasubiria kiasi cha fomu 170 kutoka katika majimbo 290 na fomu nyingine 1000 kutoka vituo 40,883 vya kupiga kura.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka wa Kenya, Wafula Chebukati amesema Alhamisi “hivi sasa tuko katika hatua za mwisho kutoa matokeo.”

“Matokeo yote ya urais kutoka kwa maafisa wa uchaguzi yatafika kwenye kituo cha majumuisho ya kura cha taifa saa sita mchana Ijumaa,” amesema Chebukati.

XS
SM
MD
LG