Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 16:30

VIJIMAMBO: Githeriman, Mkenya aliyepiga kura akibeba chakula


#Githeriman. Mkenya mmoja alibeba Githeri akiwa foleni ili kukabiliana na njaa.

Matin Kamotho, alipanga foleni siku ya Jumanne kwenye kituo kimoja katika eneo la Kayole, Nairobi, ambapo alihisi njaa na kuamua kununua Githeri kilichowekwa kwenye karatasi ya plastiki na kurejea tena kwenye laini, huku akiendelea kula chakula chake bila kujali waliokuwa wanamwangalia.

Lakini mmoja wa waliokuwa foleni naye, alimpiga picha na kuituma kwa rafiki yake ambaye aliiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Muda mfupi baadaye, picha ya Kamotho iliyokarabatiwa kwa njia ya photoshop huku ikimuonyesha akiandamana na watu maarufu ulimwenguni - kama vile Baba Mtakatifu na wengineo - ilianza kusambaa kwa kasi mitandaoni.

Vyombo vingi vya habari vilianza kumtafuta mtu huyo ili kumhoji. Sauti ya Amerika pia ilifuatilia habari hiyo na kutaka kujua zaidi kuhusu mtu huyo.

Sikiliza taarifa hiyo kati ya zingine za kustaajabisha kuhusu uchaguzi nchini Kenya katika kipindi cha Vijimambo naye mwanahabari wa VOA, BMJ Muriithi:

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:28 0:00

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG