Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:50

Kamera mpya ya utafiti wa anga za juu yarushwa kutoka French Guiana


Roketi ya Ariane 5 ikiwa na kamera ya James Webb Space ya NASA, ikiruka Jumamosi, Disemba 25, 2021, huko Ulaya katika Kituo cha Anga za Juu cha Guiana huko Kourou, French Guiana. (NASA via AP)
Roketi ya Ariane 5 ikiwa na kamera ya James Webb Space ya NASA, ikiruka Jumamosi, Disemba 25, 2021, huko Ulaya katika Kituo cha Anga za Juu cha Guiana huko Kourou, French Guiana. (NASA via AP)

Kamera ya James Webb Space ya NASA, iliyotengenezwa kuiwezesha dunia kufahamu ulimwengu ulivyokuwa wakati sayari za kwanza zilipopatikana, ilizinduliwa kwa njia ya roketi mapema Jumamosi kutoka pwani ya Kaskazini mashariki, Kusini mwa Marekani, ikifungua ukursa mpya wa enzi ya anga za juu.

Kamera hiyo iliyoleta mageuzi makubwa yenye thamani ya dola bilioni 9, imesifiwa na NASA kama ni kifaa cha kisayansi cha thamani ya juu cha uchunguzi wa anga kwa muongo ujao, kilibebwa katika eneo la mizigo la roketi Ariane 5 iliyoruka majira ya saa 11:20 asubuhi EST (1220 GMT) kutoka katika kituo cha kurushia roketi cha Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) huko French Guiana.

Picha ya kuchora inayoonyesha namna kamera ya James Webb Space inavyoonekana inapokuwa angani. (Image Credit: NASA GSFC/CIL/Adriana Manrique Gutierrez)
Picha ya kuchora inayoonyesha namna kamera ya James Webb Space inavyoonekana inapokuwa angani. (Image Credit: NASA GSFC/CIL/Adriana Manrique Gutierrez)

Urushaji wa roketi uliofanikiwa Siku ya Krismas, na kuhesabiwa kwa lugha ya Kifaransa, ulifanyika hadharani kupitia matangazo yaliyorushwa katika tovuti ya NASA-ESA.

Baada ya dakika 27 ya kusafiri katika anga, kifaa hicho chenye uzito wa paundi 14,000 kiliachiwa kutoka sehemu ya juu ya roketi iliyotengenzwa Ufaransa, na pole pole itajiachia kufikia ukubwa wa kiwanja cha tennis katika kipindi cha siku 13 kikiwa kinaelea chenyewe.

Picha za Video zilizonaswa na kamera zilizopo katika upande wa juu wa roketi hiyo zilionyesha chombo hicho kikisogea polepole kuelekea juu kutoka ardhini wakati kilipoachiwa kuruka. Wadhibiti wa safari hiyo wamethibitisha muda mchache baadae kuwa nishati ya chombo cha Webb ilikuwa inafanya kazi.

Kikiwa kinatembea katika anga kwa wiki mbili zaidi, kamera ya chombo cha Webb kitawasili katika kituo chake katika eneo la sayari ya jua lililoko maili milioni 1 kutoka Ardhini – takriban umbali mara nne zaidi kutoka mwezini.

XS
SM
MD
LG