Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:06

Kabila atishia kuwashitaki waliyomhusisha na wizi wa milioni za dola


Aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila
Aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila

Aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, amesema anapanga kushtaki shirika la habari na shirika lisilo la kiserikali kwa kusema kwamba aliiba kiasi cha dola milioni 138 katika muda wa miaka mitano akiwa madarakani.

Kabila amesema kwamba ripoti hiyo ilimharibia jina.

Ripoti hiyo ya shirika la habari za uchunguzi la Ufaransa – Mediapart, kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la kuwalinda watu wanaotoa habari za siri Afrika, inataja Kabila na watu kutoka ukoo katika kashfa ya wizi wa mamilioni kadhaa ya dola.

Wakili wa Kabila Raphael Nyabirungu amesema kwamba watafungua kesi mahakamani.

Washirika wa karibu wa Joseph Kabila wamedai kwamba rais huyo wa Zamani ni mtu mwadhilifu anayependa sana taifa lake na aliyefanya kazi kwa heshima na taadhima na kwa hivyo watamtetea kwa njia zote.

XS
SM
MD
LG