Ni matumaini yake kuwa mshikamano huo utaleta amani kati ya Waisraeli na Wapalestina, pia huko Syria na Yemeni ambako hakuna amani kutokana na vita.
Jinsi Krismasi inavyo sherehekewa nchi mbalimbali duniani
Katika ujumbe wa sikukuu ya Krismasi kwa wakazi wa Vatican na Ulimwengu mzima, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis awahamasisha watu wa mataifa yote na tamaduni mbalimbali kushikamana na kudumisha umoja.
5
Watoto wa Kikristo nchini Pakistani wakiimba mwimbo katika kanisa la mtakatifu Patriki kabla ya sherehe za Krismasi mjini Karachi, Pakistani, Jumamosi, Disemba 22, 2018.
6
Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis akitoa ujumbe maalum wa Krismas kwa wakazi wa Vatican na watu wote duniani ikiwa ni salaam za heri ya Krismas kutoka dirisha kuu la Kanisa la Mtakatifu Petro huko mjini Vatican, Jumanne, Disemba. 25, 2018.
7
Waumini wa Palestina wakiwa katika paredi wakati wa maadhimisho ya Krismasi katika eneo la Manger Square nje ya Kanisa huko Bethlehem, katika eneo lilioko chini ya utawala wa Israeli Ukanda wa Magharibi, Disemba 24, 2018.
8
.Wachungaji wakihudhuria sherehe za Krismasi katika eneo la Manger Square nje ya Kanisa huko Bethlehem, katika eneo lilioko chini ya utawala wa Israeli Ukanda wa Magharibi , Disemba 24, 2018.