Ni matumaini yake kuwa mshikamano huo utaleta amani kati ya Waisraeli na Wapalestina, pia huko Syria na Yemeni ambako hakuna amani kutokana na vita.
Jinsi Krismasi inavyo sherehekewa nchi mbalimbali duniani
Katika ujumbe wa sikukuu ya Krismasi kwa wakazi wa Vatican na Ulimwengu mzima, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis awahamasisha watu wa mataifa yote na tamaduni mbalimbali kushikamana na kudumisha umoja.
1
Mchungaji nchini Syria akiongoza ibada ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Maria huko mjini Diyarbakir, Uturuki, Disemba 25, 2018.
2
Prince Charles, Prince William, Duke wa Cambridge na Catherine, Duchess wa Cambridge akiwa na Prince Harry, Duke wa Sussex and Meghan, Duchess wa Sussex wakiwasili katika kanisa la mtakatifu Maria Magdalena kwa ibada ya Krismasi iliyoandaliwa kwa ajili ya familia ya kifalme Uingereza.
3
Wanajeshi wa Marekani na Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO ) wakiimba nyimbo za Krismasi wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Krismasi huko katika ofisi zake zinazo fanya usimamizi wa vikosi hivyo mjini Kabul, Afghanistan, Disemba 25, 2018.
4
Rais Donald Trump akiwasikiliza wanajeshi wa vikosi vitano vya jeshi wakati akifanya maongozi nao siku ya Krismas, Disemba 25, 2018, katika ofisi yake ndani ya White House. Wanajeshi hao wako nchini Guam, Qatar na Alaska na makundi mawili yako Bahrain.