Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 07:06

Je, nini kilichosababisha kuvurugika matumaini ya wananchi wa Sudan?


Je, nini kilichosababisha kuvurugika matumaini ya wananchi wa Sudan?
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:39 0:00

Mwezi Aprili 2019, maelfu ya watu walijaa katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kusherehekea kuondolewa kwa dikteta wa muda mrefu Omar al-Bashir. Kulikuwa na matumaini kwamba nchi ilikuwa inaingia katika enzi mpya.

Waziri mkuu wa serikali ya kiraia, Abdalla Hamdok, aliteuliwa kuongoza serikali ya mpito iliyoundwa na raia na wanajeshi. Lengo lilikuwa kujiandaa kwa uchaguzi na kuirudisha nchi hiyo kwenye demokrasia.

Lakini kufikia mwaka 2021, mipasuko iliibuka. Uchumi wa nchi ulikuwa katika hali mbaya,mfumuko wa bei uliongezeka kwa asilimia 400 na uhaba wa mahitaji muhimu kama mkate. Jeshi lilidhibiti sekta kubwa za uchumi, zikiwemo mabenki, migodi na mashirika ya kilimo. Wanajeshi walikataa kuachia mamlaka.

Hamdok na raia wengine walipojaribu kuanzisha mageuzi, uongozi wa kijeshi ulipinga. Tarehe 25 Oktoba 2021, Hamdok aliwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani, na muda mfupi baadaye, majenerali wawili walichukua mamlaka.

Mmoja wao ni, Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kwa jina la Hemedti, aliyeongoza kikosi cha Rapid Support Forces, kikundi cha wanamgambo maarufu kwa ukatili wake.

XS
SM
MD
LG