Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:07

Je, Facebook iko tayari kwa uchaguzi wa Marekani 2020?


Tangu majasusi wa Russia na wengine wenye maslahi binafsi walipotumia vibaya safu yao katika mtandao wa Facebook kwa ajili ya kuingilia kati uchaguzi wa Marekani 2016, Facebook imesisitiza mara kwa mara kuwa imepata fundisho na haitakuwa tena uwanja wa kupitisha taarifa za uongo, ukandamizaji kwa wapiga kura na kuvuruga uchaguzi.

Lakini imekuwa safari ndefu na yenye kusuasua kwa mtandao huo wa kijamii, linaeleza shirika la habari la AP.

Wakosoaji wake, na pia baadhi ya wafanyakazi wa Facebook, wanasema juhudi za kampuni hiyo kurekebisha kanuni na kuweka vizuizi zaidi vimekuwa na mianya isiyowezesha kutekelezwa, hata baada ya kutumia mabilioni kwa ajili ya mradi huo.

Na wanatoa sababu, kwa kuonyesha kuendelea kwa kampuni hiyo kutokuwa tayari kuchukua maamuzi kwa yale yaliopita wakati ule.

“Nina wasiwasi juu ya uchaguzi huu? Inaniogopesha,” amesema Roger McNamee, mzalishaji mshiriki katika biashara huko Silicon Valley na mwekezaji wa awali wa Facebook ambaye amekuwa mkosoaji. “Kwa nafasi ya kampuni hiyo hivi sasa, ni hatari iliyodhahiri kwa demokrasia na usalama wa taifa.”

Matamko ya kisiasa ya kampuni hiyo bila shaka yamepatiwa maelezo mapya.

Mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg hivi sasa mara kwa mara anaelezea uwezekano wa kutokea mambo ambayo hayakufikiriwa mwaka 2016 – kati ya hayo, uwezekano wa ghasia za kiraia na kuwepo kwa mvutano wa matokeo ya uchaguzi ambapo Facebook kwa urahisi kabisa inaweza kufanya hali hiyo kuwa mbaya – kama changamoto ambazo mtandao huo unakabiliwa nazo.

Mark Zuckerberg akihojiwa na Kamati ya Huduma za Fedha ya Baraza la Wawakilishi Capitol Hill, Washington, Oct. 23, 2019.
Mark Zuckerberg akihojiwa na Kamati ya Huduma za Fedha ya Baraza la Wawakilishi Capitol Hill, Washington, Oct. 23, 2019.

“Uchaguzi huu hauwezi kuwa wa hali ya kawaida,” Zuckerberg ameandika katika ujumbe wake katika Facebook mwezi Septemba akiorodhesha juhudi zinazofanywa na Facebook kuhamasisha upigaji kura na kuondoa taarifa za uongo kutoka katika mtandao wake. “Sote tunalojukumu la kulinda demokrasia yetu.”

Hata hivyo kwa miaka kadhaa watendaji wa Facebook walionekana kutokuwa wamejiandaa pale mtandao wao – uliowekwa kuiunganisha dunia – ulipotumika kwa ajili hujuma mbalimbali.

Zuckerberg ameomba radhi mara nyingi kwa miaka kadhaa, kana kwamba hakuna mtu aliyekuwa anaweza kutabiri kuwa watu wangetumia mtandao wa Facebook kuonyesha mauaji mubashara na kujiua, kuhamasisha mauaji ya halaiki, kusambaza matibabu ya uongo ya saratani au kujaribu kughushi matokeo ya uchaguzi.

Wakati mitandao mingine kama Twitter na You Tube imejaribu kutatua suala la maudhui potofu na chuki , Facebook ina mtandao mkubwa wenye wafuasi wengi, ikilinganishwa na mitandao mingine, hali yake ya kukabiliana na changamoto zilizotambuliwa mwaka 2016 kuwa inakwenda polepole.

Na matokeo ya hapohapo katika uchaguzi wa Rais Donald Trump, Zuckerberg alinyamazia kuhusu tetesi kuwa “habari potofu” zinazosambazwa katika Facebook zingeweza kuingilia kati uchaguzi wa mwaka 2016, akisema “ ni fikra isiyokuwa ya kawaida.” Wiki moja baadae, akarekebisha usemi huo.

Social media logo
Social media logo

Tangu wakati huo, Facebook imeomba radhi mara kadhaa kwa kutochukua hatua haraka dhidi ya vitisho hivyo vya uchaguzi wa 2016 na kuahidi kurekebisha hali hiyo.

“Sidhani wamekuwa wasikilizaji wazuri,” amesema David Kirkpatrick, mtunzi wa kitabu “Facebook’s rise. “Kilichobadilika ni kuwa watu wengi zaidi wamekuwa wakiwaambia wanatakiwa kuchukua hatua fulani.”

Kampuni hiyo imeajiri watu kuhakiki habari iwapo ni za kweli, na kuongeza makatazo – na makatazo zaidi – katika matangazo ya kisiasa na kufunga maelfu ya akaunti, kurasa na vikundi viligundulika kujihusisha “kuratibu tabia zisizo kuwa za kawaida.”

Hayo ndio maelezo ya Facebook kwa akaunti na vikundi feki katika Facebook ambavyo vinalenga kuhujumu mazungumzo ya kisiasa katika nchi mbalimbali kutoka Albania hadi Zimbabwe.

Pia ilianza kuweka alama za tahadhari kwa ujumbe ambao una taarifa potofu kuhusu kupiga kura na mara nyingine, imechukua hatua kupunguza usambazaji wa taarifa potofu.

Katika wiki za karibuni mtandao huo pia ulipiga marufuku ujumbe uliokuwa ukikanusha mauaji ya Holocaust na kuungana na Twitter kupunguza usambazaji wa habari za kisiasa zilizokuwa hazijathibitishwa juu ya Hunter Biden, mtoto wa mgombea urais wa chama cha Demokratik Joe Biden, uliochapishwa na gazeti la kiconservative New York Post.

Yote haya hayapingiki yanaiweka Facebook katika nafasi bora zaidi kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Lakini hilo halimaanishi kuwa wamejitayarisha kikamilifu.

Pamoja na kuwepo kanuni madhubuti zinazozuia habari potofu, vikundi vya wanamgambo wenye ghasia vinaendelea kutumia mtandao huo kuandaa harakati zao. Hivi karibuni, maandalizi hayo yamehusisha jaribio la kutaka kumteka gavana wa jimbo la Michigan.

“Kipaumbele chao Facebook ni kukuza biashara yao, na sio kupunguza madhara yanayotokana na Facebook,” Kirkpatrick amesema. “Na hilo siyo rahisi kubadilika.”

Sehemu ya tatizo hilo : Zuckerberg anasisitiza inaudhibiti wa nguvu wa kampuni hiyo, lakini haichukulii ukosoaji dhidi yake au kampuni yake kwa makini, mtaalam wa mitandao ya kijamii anadai Jennifer Grygiel ambaye ni Mhadhiri wa mwasiliano wa Chuo Kikuu cha Syracuse.

Lakini umma unafahamu kile kinachoendelea, amesema. Wanaona jinsi Donald Trump anavyoitumia vibaya. Hawawezi kupuuza.”

Facebook imesisitiza inachukua hatua za dhati kupambana na habari potofu – hususan wakati wa uchaguzi.


XS
SM
MD
LG